Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Bora unifunge ila sio kunizidi soka safi

Gamondi Yanga Yake Gamondi: Bora unifunge ila sio kunizidi soka safi

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Gamondi amesema kuwa falsafa ya soka lake ni la kuburudisha hata kama itatokea anapoteza mchezo.

Gamondi ameingia kwenye vitabu vya Historia mpya ya Klabu ya Wananchi Yanga SC kwa kushinda bao 5 katika mechi nane ndani ya msimu wake wa kwanza tu kwenye timu hiyo.

"Ni bora unifunge kuliko nikuonyeshe udhaifu tena nyumbani kwangu, mimi mpira ni burudani nataka niburudishe halafu nishinde, ikitokea nimeshindwa basi nitakuwa nimeburudisha na ikitokea nimeshinda na kuburudisha pia.

"Siwezi kucheza na mabeki 9 halafu mshambuliaji mmoja hata kama naongoza kwa mabao matano nitaendelea kukushambulia tu," amesema Kocha Miguel Gamondi.

◉ Yanga 5 - 0 KMC

◉ Yanga 5 - 0 JKT Tanzania

◉ Yanga 5 - 1 ASAS

◉ Yanga 5 - 1 Simba SC

◉ Yanga 5 - 0 Jamhuri

◉ Yanga 5 - 1 Hausing FC

◉ Yanga 5 - 0 Polisi Tanzania

◉ Yanga 5 - 0 Ihefu FC.

Mechi inayofuata ni Yanga dhidi ya Geita Gold FC.

Pengine Miguel Gamondi ndiye kocha katili zaidi kwenye historia ya Yanga SC?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: