Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Baadhi ya Wachezaji wangu ni majeruhi

Miguel Gamondi Maboa Kesho Miguel Angel Gamondi, Kocha wa Yanga

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Yanga ikijiandaa kuivaa Ihefu katika mchezo wa mzunguko wa nne wa Ligi Kuu Tanzania Bara Oktoba 4 Jijini Mbeya.

Kocha Mkuu wa Kikosi hicho, Miguel Gamondi amesema kuwa baadhi ya nyota wake wanasumbuliwa na majeraha hivyo wanaweza kuukosa mchezo huo.

akiwa bado hajaweka wazi majina ya wachezaji hao Gamondi amesema kuwa wanatazama maendeleo ya wachezaji wote katika mazoezi ya mwisho leo jioni ili kujua nani atakuwa tayari kwa mchezo.

Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari Gamondi amesema;

"Wachezaji wako kwenye hali nzuri na morali yao iko juu, kuna baadhi ya wachezaji wana majeraha lakini tutajua kwenye mazoezi ya mwisho leo jioni ni wachezaji wapi watakuwa sawa kwa ajili ya mchezo wa kesho" Gamondi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: