Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gallagher azikataa Atletico, Tottenham, Aston Villa

 Conor Gallagher F Gallagher azikataa Atletico, Tottenham, Aston Villa

Thu, 20 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo wa Chelsea, Conor Gallagher amewaambia mabosi wa timu hiyo kwamba hawatamlazimisha kuondoka katika dirisha hili kwani bado anaamini ana nafasi ya kupambana katika kikosi cha kwanza cha wababe hao wa darajani.

Conor ambaye anawindwa na Atletico Madrid, Aston Villa na Tottenham, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2025.

Licha ya Chelsea kutaka kumuuza Conor ni mmoja kati ya wachezaji walioonyesha kiwango bora katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kwa msimu uliopita.

Matajiri hawa wa Jiji la London wanataka kumuuza kwa ajili ya kujipatia pesa ambazo zitawaweka katika hali nzuri ya kiuchumi kutokana na kesi zinazowakabili.

Msimu uliopita staa huyu wa kimataifa wa England amecheza mechi 51 za michuano yote, amefunga mabao saba na kutoa asisti tisa.

Gallagher alionyesha kiwango bora kabisa msimu wa 2021–2022 wakati akiitumikia kwa mkopo klabu ya Crystal Palace akitokea Chelsea ambayo alijiunga nayo tangu akiwa kinda mwaka 2008.

ARSENAL imeachana na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia, Benjamin Sesko, 21, katika dirisha hili na badala yake inaangalia uwezekano wa kusajili kiungo kwa ajili ya kuboresha eneo hilo.

Sesko ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2029, alishindikana kutua Arsenal baada ya timu yake kumuongeza mkataba mpya na kuhitaji kiasi kikubwa cha pesa.

MPANGO wa Manchester United kumsajili straika wa Bologna na Uholanzi, Joshua Zirkzee katika dirisha hili unakwamishwa na kiasi kikubwa cha pesa ambacho timu yake inakihitaji ili kumuuza staa huyo.

Inaelezwa Bologna inahitaji zaidi ya Euro 60 milioni pamoja na nyongeza ili kumwachia Zirkzee mwenye umri wa miaka 23. Mkataba wake unamalizika mwaka 2026.

WINGA wa Manchester United na Ivory Coast, Amad Diallo, 21, anatarajiwa kuingia katika mazungumzo na mabosi wa timu hiyo kwa ajili ya kusaini mkataba mpya utakamwezesha kudumu kwenye timu hiyo kwa muda mrefu zaidi.

Staa huyu anaongezwa mkataba mpya kutokana na maagizo ya kocha wa timu hiyo Erik ten Hag ambaye bado yupo katika mipango yake.

ARSENAL imeanza mazungumzo na wawakilishi wa kipa wao namba tatu, Estonian Karl Hein, 22, kwa ajili ya kumsainisha mkataba mpya utakaomwezesha kusalia kaika timu hiyo kwa muda mrefu zaidi.

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kwamba kipa huyu huenda akandoka kwa mkopo kwenda timu itakayompa nafasi ya kucheza zaidi katika kikosi cha kwanza.

TOTTENHAM na Arsenal zinadaiwa kuwa miongoni mwa timu zinazomfuatilia kwa muda mrefu kiungo wa Juventus na Marekani, Weston McKennie na zinataka kuwasilisha ofa katika dirisha hili jambo litakaloivurugia Aston Villa iliyo katika mazungumzo na wawakilishi wake ili kumsajili. Weston mwenye umri wa miaka 25, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2025.

MSHAMBULIAJI wa Juventus, Federico Chiesa yupo katika orodha ya wachezaji ambao Bayern Munich inahitaji kuwasajili katika dirisha hili. Inaelezwa Bayern imekuwa ikimfuatilia fundi huyu wa kimataifa Italia kwa muda mrefu na hivi karibuni imepanga kuwasilisha ofa baada ya kuona mkataba wake umebaki mwaka mmoja kumalizika.

Juventus inahitaji kati ya Pauni 27 na 35 milioni ili kumuuza.

MAZUNGUMZO baina ya Tottenham na Bologna juu ya beki wa timu hiyo na Italia, Riccardo Calafiori yamefikia pazuri na kuna uwezekano dili hilo likakamilika katika dirisha hili

Calafiori, 22, alikuwa chachu ya kufanya vizuri kwa Bologna kwa msimu uliopita kwenye Ligi Kuu Italia.

Licha ya mazungumzo hayo kwenda vizuri hadi sasa bado hakuna muafaka wowote uliofikiwa baina ya pande zote mbili kuhusiana na ada ya uhamisho.

Chanzo: Mwanaspoti