Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gallagher aitaka Atletico Madrid

 Conor Gallagher F Kiungo na nahodha wa Chelsea, Conor Gallagher

Thu, 1 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo na nahodha wa Chelsea, Conor Gallagher amekataa mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia timu hiyo ya Darajani na tetesi zinasema huenda akatimkia Atletico Madrid dirisha.

Kwa mujibu wa taarifa, Gallagher amekataa ofa hiyo na tayari ameshawaambia mabosi anataka kujiunga na Atletico ambayo imeshawasilisha ofa ya Pauni 33 milioni ili kukamilisha dili hilo.

Gallagher, ambaye alijiunga na akademi ya Chelsea akiwa na umri wa miaka minane, pia aliwahi kukataa mkataba mpya aliopewa Juni mwaka huu.

Staa huyu amekuwa akihusishwa kuwa sokoni na Chelsea kwa muda mrefu kwa kile kinachoelezwa inataka kuweka sawa vitabu vyao vya hesabu ili kuendana na sheria za matumizi ya fedha ya Ligi Kuu England.

Gallagher pia alikataa ofa zilizowekwa mezani na Aston Villa na Tottenham Juni mwaka huu, kwa sababu kiungo huyu anataka kujiunga na timu itakayompa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa.

Hata hivyo, licha ya ripoti kudai Atletico imefikia makubaliano na Chelsea, timu hiyo itatakiwa kuuza mchezaji mmoja mara baada ya kumsajili Gallagher ili kuweza kulipa ada yake ya uhamisho.

Gallagher amebakiza mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake na Chelsea haitaki kumpoteza bure mwakani, hivyo baada ya kukataa kusaini dili jipya imeamua bora imuuze.

Kwa sasa fundi huyu yupo mapumzikoni baada ya kuitumikia England katika michuano ya Euro kule Ujerumani.

Chanzo: Mwanaspoti