Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Galatasaray yapanga kumsajili Zaniolo

Nicolo Zaniolo Nicolo Zaniolo

Mon, 6 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa Okan Buruk wa klabu ya Galatasaray amesema kuwa wana mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Roma Nicolo Zaniolo katika siku za mwisho za dirisha la uhamisho la Uturuki.

Huku kukiwa na nia ya mabingwa watetezi wa Serie A, Milan, Zaniolo alielezea nia yake ya kuondoka Roma mwezi uliopita, lakini mchezaji huyo wa Kimataifa wa Italia alichukizwa na uongozi wa klabu hiyo kwa kukataa uhamisho wa kuhamia kwa klabu ya ligi kuu Bournemouth ambayo aina mwendelezo mzuri.

Jose Mourinho alielezea uwezekano wa Zaniolo kusalia Roma kama bahati mbaya muda mfupi kabla ya dirisha la vilabu vingi vya Ulaya kufungwa, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 bado anaweza kukamilisha uhamisho huo.

Huku kukiwa na ripoti zinazosema kuwa Galatasaray wako kwenye mazungumzo ya kuweka mkataba wa zaidi ya Euro milioni 22 kwa Zaniolo, Buruk alimsifu Muitaliano huyo.

Buruk amesema kuwa; “Zaniolo ni mchezaji wa kiwango cha Kimataifa na aliyasema hayo baada ya ushindi wa 2-1 wa Galatasaray dhidi ya Trabzonspor. Ni mchezaji ambaye tungependa kumuona kwenye kikosi, hata kama hatujui kabisa uhusiano wake na Roma.”

Lakini ukiniuliza, unataka kumuona kwenye timu?’ Bila shaka, ningependa kuwa naye. Alimalizia hivyo kocha huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live