Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gadiel atoa somo mastaa wanaokaa benchi Simba, Yanga

Gadiel Michael Msg Gadiel atoa somo mastaa wanaokaa benchi Simba, Yanga

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki Gadiel Michael aliyejiunga na Cape Town ya Afrika Kusini, ametoa somo kubwa kwa mastaa wa Simba, Yanga wanaokaa benchi.

Gadiel ni kati ya wachezaji waliobahatika kucheza klabu zote tatu kubwa hapa nchini, Azam FC (2014-2017), Yanga (2017-2019) na Simba (2019-2023) na baadaye akaibukia Singida Fountain Gate.

Hivi Karibuni, Singida ilitangaza kuwa staa huyo ameondoka klabuni hapo na atajiunga na Cape Town ya Afrika Kusini kwa mkopo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mastaa wa zamani wa soka wamesema beki huyo ni mfano sahihi wa vijana ambao hawapo tayari viwango vyao kufia Simba na Yanga pekee.

Staa wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Zamoyoni Mogella amesema Gadiel amefanya kitu ambacho kimekuwa wimbo wake wa muda mrefu kwa vijana wengi, kuangalia pesa wanazokalia benchi kwenye klabu kongwe.

"Mitazamo ya vijana wengi ndio inayoua vipaji vyao, mfano mzuri ni Gadiel baada ya kujiunga Simba akitokea Yanga alikuwa na jina kubwa, kutokana na kukosa nafasi akaonekana wa kawaida kabisa hadi akapoteza namba kwenye kikosi cha Stars, baada ya kutoka milango mingine inafunguka.

"Soka ni kazi yao, lazima wajifunze kuthubutu na waache kuridhika, wakati wanaweza wakapata pesa nyingi kwenye soka la sasa ambalo ni biashara."

Kipa wa zamani wa Simba na Yanga, Ivo Mapunda amesema; "Mchezaji akijiamini anachokifanya anakuwa na nafasi kubwa ya kuweka uwanja mpana wa kufanya kazi zake, naamini Gadiel ataongeza kujiamini na atakuwa bora zaidi huko mbele."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live