Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gadiel aache kutia huruma - Mchambuzi

Gadiel Michael Msg Gadiel aache kutia huruma - Mchambuzi

Mon, 6 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji na mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Fradius Mugoa amesema kuwa beki wa Singida Fountain Gate FC, Gadiel Michael aache kutia huruma kwa kudai alifanyiwa figisu Simba akaamua kuondoka.

Gadiel hivi karibuni alidai kuwa alikuwa amechelewa kuondoka Simba huku akidai kuwa alifanya kosa kubwa kuondoka Yanga.

"Gadiel Michael alipata nafasi Azam FC baadaye akaomba kuondoka kwenda Yanga baadaye Yanga akawasumbua mpaka kuwazimia simu akahamia Simba.

"Hivyo kwa sasa asitie huruma kwa sababu hata angekuwepo Yanga hii asingepata nafasi. Singida FG tu bado hana uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza Yanga hii asingepenya mbele ya Lomalisa na Kibabage," amesema Mugoa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: