Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gadiel Michael: Kutoka kwenye mashamba ya Alizeti mpaka kwa Madiba

Gadiel Michael Kamagi.jpeg Gadiel Michael.

Sat, 9 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Ernst Middendorp akiwa Singida alimchezesha Gadiel Michael katika eneo la kiungo katika mfumo wake mama wa 3-4-3 badala ya kumchezesha kwenye nafasi yake beki wa kushoto kama ilivyozoeleka miaka yote.

Timu ikiwa inashambulia Gadiel anakuwa anaingia ndani kama kiungo kusaidiana na viungo wa kati lakin akisogea mbele kama wing back.

Lakini timu ikiwa haina mpira anaungana na Mabeki wake kutengeneza ngome ya Mkwawa, ngome ngumu na Gadiel ali-react vyema na kuonyezha kiwango bora sana.

Mechi moja ambayo Gadiel alionyesha kiwango bora sana ndiyo mechi iliyopelekea kocha huyo kuondoka akijata sababu mojawapo ni kwamba viongozi wanampangia nani acheze wapi na nani aanze kwenye kikosi.

Kocha akataja kuwa sababu ya kumchezesha Gadiel Michael nafasi ya kiungo ni kutokana na uwezo wake aliovutiwa nao, hakuacha kumtaja kama mchezaji wake aliyevutiwa naye.

Mara baada ya kuondoka na kurudi zake Afrika Kusini, baadae akateuliwa kuwa kocha Mkuu wa Cape Town Spurs, katika dirisha dogo akarudi kumfuata mwanae Gadiel.

Tunapozungumza Gadiel ni panga pangua kwenye kikosi cha kwanza cha Cape Town, juzi kaweka dhidi ya Orlando Pirates.

Wanasema siku Mungu akiamua kukufungulia njia huwezi jua itakuwaje lakini hakuna wa kukuzuia kama wakati wa Mungu ukifika. Gadiel endelea kuwasha moto huko mpaka wakutaftie AKA yao huko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live