Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gabriel Jesus airudisha sokoni Arsenal

Jesus Gabriel Gabriel Jesus airudisha sokoni Arsenal

Fri, 23 Dec 2022 Chanzo: Dar24

Meneja wa Klabu ya Arsenal Mikel Arteta, amewatoa wasiwasi Mashabiki wa klabu hiyo kuelekea Dirisha Dogo la Usajili (Mwezi Januari 2023), kwa kusema atafanya usajili wenye malengo ya kuendelea kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya England na Europa League.

Arsenal itamkosa Mshambuliaji wake kutoka Brazil Gabriel Jesus kwa zaidi ya mwezi mmoja, baada ya kuumia akiwa katika majukumu ya Timu ya Taifa wakati wa Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar.

Jesus, alisajiliwa na The Gunners mwanzoni mwa msimu huu akitokea Manchester City, alipatwa na majeraha wakati wa mchezo wa mwisho wa Hatua ya Makundi dhidi ya Cameroon, iliyoibuka na ushindi wa 1-0.

Arteta amesema hana budi kuingia sokoni ili kusajili, na anaamini mambo yatakua mazuri kutokana na namna alivyojipanga msimu huu, ambapo hadi sasa Arsenal inaongoza katika Msimamo wa Ligi Kuu.

Amesema anafahamu haitakuwa rahisi kwa kikosi chake kucheza bila Mshambuliaji Jesus aliyezoeleka tangu mwanzoni mwa msimu huu, lakini bado akasisitiza kuwa, Usajili wa Dirisha Dogo ndio suluhisho la kumaliza changamoto inayowakabili.

“Nafahamu haitakuwa rahisi, itachukua muda kuwa na mtu kama Jesus katika kikosi, lakini hili linapaswa kuchukuliwa kama changamoto ambayo itatujenga ili kufanikisha lengo linalokusudiwa, mwishoni mwa msimu.

“Hakuna aliyetarajia kama angeumia, lakini imetokea na ameshaumia, njia rahisi ni kuhakikisha pengo lake linazibwa wakati wa Dirisha Dogo, ninaamini kwa kushirikiana na wenzangu tutampata Mshambuliaji ambaye atatupa matokeo na kuweza kufanya vizuri kwenye michezo yetu.

“Tunapaswa kuendelea kuwa na matokeo mazuri, hatupaswi kushuka chini na kurejea kule ambako Mashabiki hawataki turudi, niwahakikishie tutasajili na tutasajili mtu sahihi,” amesema Arteta.

Arsenal inaongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa alama tano dhidi ya Mabingwa watetezi Manchester City, na inatarajia kurejea kwenye mipango ya kutetea nafasi yake hadi kufikia lengo la kutwaa ubingwa Desemba 26 kwa mchezo dhidi ya West Ham United.

Chanzo: Dar24