Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

GSM ndiye alinishawishi kujiunga na Yanga

Manara GSM GSM ndiye alinishawishi kujiunga na Yanga

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyewahi kuwa msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa alianza kuichukia klabu hiyo mara tu baada ya kuondoka na kujiunga na watani zao Yanga SC, mwwanzoni mwa msimu wa 2021/2022.

Baada ya kutofautiana na baadhi ya viongozi wa Simba kisha kuondolewa klabuni hapo, Manara amesema alijiunga na Yanga baada ya kupigiwa simu na mdhamini wa klabu hiyo, mfanyabiashara Ghalib Said Mohammed (GSM) na kumtaka ajiunge na Wananchi.

“Ghalib (GSM) aliniambia kama utani kwamba mimi nikikupata wewe yaani hawa Simba hawajui kabisa kukutumia.

“Kwenye mazungumzo Ghalib akanitania kama atafurahi tukifanya kazi pamoja mimi nikawa naona utani lakini baada ya yale matukio ndio ikawa hivyo kwahiyo siku niliyotoka Simba ndio siku nilianza kuichukia Simba,” amesema Haji Manara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: