Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

GSM haijatoa fedha kwa Vilabu, Je wana lengo gani?

FK  QDeWQAMR Ht Fedha za GSM zazua gumzo kwa vilabu

Tue, 8 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya GSM iliingia Mkataba na Shirikisho la Soka nchini TFF, la udhamini mwenza Ligi Kuu ya NBC, kwa muda wa miaka miwili Mkataba wenye thamani ya Bilioni 2.1

Hiyo ilikuwa November 23, 2021 udhamini ambao ulikuwa na vipengele mbali mbali vya kumfaidisha mdhamini ikiwemo kuvaa nembo ya mdhamini katika bega la Kushoto na kuweka mabango yasiyopungua manne kuzunguka Uwanja.

Vilabu 15 vya Ligi Kuu vilikubali Masharti hayo isipokua Simba SC ambao walitaka maelezo zaidi kuhusiana na Mkataba huo.

Vilabu 15 vilishaanza kutekeleza hatua hiyo, ya kuvaa nembo ya mdhamini na kutandaza mabongo Uwanjani.

Sasa jana Februari 7, GSM ilitangaz kuvunja Mkataba huo wa udhamini mwenza kutokana na kile walichodai TFF na Bodi ya Ligi kukiuka baadhi ya vipengele vya Mkataba huo.

Sasa taarifa za uhakika zinasema mpaka kufikia jana, Februari 7, GSM walikua hawajatoa kiasi chochote cha fedha katika Mkataba waliokuwa wamekwishaingia licha ya kuwa tayari vilabu 15 kati ya 16 vinavyoshiriki Ligi Kuu NBC vilishaanza kutekeleza agizo hilo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Steven Mguto amesema Suala hilo limekaa Kisheria hivyo watakaa na kuitazama barua hiyo kisha watakuja na kauli juu ya jambo hilo.

Ziko taarifa zinazodai kuwa GSM walipaswa walipe fedha kuanzia Januari mwaka huu, sasa swali ni je watatoa fedha kwa kipindi chote ambacho klabu wamevaa nembo ya mdhamini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live