Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

GMS naye alikuwepo kushuhudia rekodi ya Yanga

Gsm Hersi Arafati (22).jpeg GMS naye alikuwepo kushuhudia rekodi ya Yanga

Sun, 1 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bosi wa Yanga Ghalib Said Mohamed 'GSM' ni miongoni mwa watu waliohudhuria mchezo wa jana kati ya Yanga dhidi ya Al Merreikh ya Sudan.

Gharib alifika Uwanja wa Azam Complex saa 11:38 jioni akiongozana na Rais wa Yanga, Hersi Said na Makamu wake Arafat Haji.

Wakati viongozi hao wakiingia ndani ya uwanja kuelekea jukwaa la viongozi mashabiki wa Yanga wamekuwa wakiwashangilia.

Mara ya mwisho kwa GSM kuhudhuria mechi ya Yanga ilikuwa ni Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika pale Uwanja wa Benjamin Mkapa walipokutana na USM Alger.

Yanga jana iliweka rekodi ya miaka 25 iliyopita kwa kutonga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuifunga Al-Merreikh bao 1-0 wakati matokeo ya jumla yakiwa ni bao 3-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live