Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

GB64 agoma kuhama Simba SC

Chama Gb 64 GB64 agoma kuhama Simba SC

Wed, 10 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki maarufu wa Klabu ya Simba, Abdulshahib Hegga maarufu kama GB64 amesema kuwa licha ya aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama kusajiliwa na watani zao Yanga SC, ametengua kauli yake ya kuwa angeacha kuishabikiwa timu yake hiyo.

GB 64 kabla ya Chama kusajiliwa Yanga SC

"Chama akienda Yanga mimi naacha kushabikia Simba yaani hiyo serious kabisa napumzika kushabikia Simba naenda Azam FC. Nakwambia Chama ukimuona hayupo ndani ya Simba ujue Simba wanasafisha timu lakini haendi Yanga anaenda nje ya nchi hii."

GB 64 baada ya Chama kutambulishwa Yanga

"Mimi kitendo cha kusema Kwamba Chama akiondoka akaenda Yanga nitaenda Azam ni kuwatuliza wana Simba ili uongozi wetu upate kutulia ufanye programm ya timu vizuri kwamba nilikuwa nawaaminisha mashabiki Chama atakuwepo kwa sababu wana Simba wananikubali GB 64, tusiendelee kuushambulia uongozi hapa akili kubwa imetumika.

"Ukweli Ni kwamba siwezi kutoka Simba nikaenda Azam. Mimi bado ninaamini Chama ni mchezaji wa Simba hadi nione tamko la uongozi wangu wakimpa 'thank you' Chama kwa sasa bado siamini hizo taarifa za Chama kwenda Yanga."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live