Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#FuuTime: Simba Sc vs Al Hilal hakuna mbabe

Simba Hilal Bn Wachezaji wa Simba wakipongezana baada ya kusawadhisha

Sun, 5 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Simba SC ya Tanzania na Al Hilal ya Sudan zimetoshana nguvu katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam baada ya kutoka sare ya bao 1-1.

Mchezo huo muhimu kwa timu zote zikijiandaa na michezo ya Klabu Bingwa Afrika ambayo inaanza kutimu vumbi juma lijalo umepigwa leo Jumapil, Januari5, 2023.

Al Hilal ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Makabi Lilepo dakika ya 6 baada ya kupasiwa mpira wa adhabu uliopigwa na Ibrahim Imoro na kuuzamisha kimyani huku akimuacha Kipa wa Simba Beno Kakolanya akiokota hewa.

Bao la kusawadhisha la Simba limefungwa na Habib Kyombo dakika ya 81 baada ya kupokea pasi ya Pape Ousmane Sakho.

Al Hilal imemaliza ratiba yake ya mechi tatu za kirafiki Nchini baada ya kutoshana nguvu na Namungo FC (1-1), ushindi dhidi Azam FC (1-0) na sare dhidi ya Mnyama (1-1).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live