Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fury ampa tano Wladimir Klitschko

Wuzupnigeria 2022 03 145d8c52 2cbd 4624 A94f 346f3e7b4b25 Fury Usyk Fury ampa tano Wladimir Klitschko

Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa ngumi uzito wa juu duniani, Tyson Fury, amewaunga mkono mabondia wa Ukraine, Wladimir Klitschko na Vitali Klitschko kwa kitendo cha kujitoa kwenda kusapoti nchi yao katika vita inayoendelea.

Mabondia hao ambao ni ndugu wamejitoa kwenda kupambania nchi yao ya Ukraine ambayo ipo kwenye vita dhidi ya Urusi.

Mwaka 2015, Fury alifanikiwa kupambana na bondia mmoja kati yao ambaye ni Wladimir Klitschko, akashinda.

Staa huyo alisema: “Kuna sheria mbili, mpende mwanamke wako na pambania nchi yako, hivyo wacha wapambanie nchi yao jambo ambalo ni muhimu, mimi niko pamoja nao.

“Kwa sababu unaweza kutafuta fedha halafu mwisho wa siku ukashindwa kurudi nyumbani na kutamba, hivyo ni bora kwenda kuipigania nchi yako. “Vijana endeleeni kupambana bila kuchoka na wala msikate tamaa, msijisalimishe, tuko pamoja.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live