Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Funga kazi ni wikiendi hii Ufaransa

Mbappe Aifungia PSG Licha Ya Kuwachwa Nje Katika Kikosi Cha Kwanza Funga kazi ni wikiendi hii Ufaransa

Fri, 17 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Siku zimewadia, viwanja 17, pale Ufaransa vitawaka moto kesho Jumapili, kuanzia saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki na vita mbalimbali zitakwenda kuamuliwa.

Kule juu kati ya timu nne zitakazoshiriki Ligi ya Mabingwa mwakani zimeshapatikana ambazo ni PSG, Monaco, Lille na Brest.

Kwa upande wa Europa League, Nice nayo imeshajihakikishia na sasa timu inayosubiriwa ni moja tu ile itakayofuzu michuano ya Uefa Conference League na Olympique na Lens ndizo zinagombania.

Lens ndio ipo nafasi ya sita inayoiwezesha kufuzu michuano hiyo lakini ina pointi 50 sawa na zile za Lyon na kinachosubiriwa ni matokeo ya mechi ya mwisho.

Ikiwa Lens itapata sare ama kufungwa na Montpelier kisha Lyon ikashinda dhidi ya Strasbourg basi Lyon itaishusha Lens.

Ikiwa zote zitashinda basi Lyon itatakiwa kufunga zaidi ya mabao manane huku ikiiombea Lens isipate bao hata moja ili wawe juu kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Kwa upande wa kushuka daraja, hadi sasa ni Lorient ama Metz moja wapo itatakiwa kuungana na Clermont katika Ligi Daraja la pili msimu ujao.

Lorient ina pointi 26 na Metz ni 29, hivyo kama Metz itapoteza mechi ya mwisho halafu Lorient ikashinda kwa zaidi ya mabao mawili basi, Metz itashuka halafu Lorient itatakiwa kwenda kucheza mechi ya mtoano itakayoamua wanabaki au la.

Lakini ikiwa ni tofauti aidha Lorient ikaambulia sare au kufungwa, basi itakuwa imeshuka na Metz itaenda kucheza mechi ya mtoano itakayoamua wanabaki au laa.

Lakini Metz pia ina nafasi ya kujitetea kutocheza mechi ya mtoano ikiwa itashinda mechi yao ya mwisho kisha Le Havre iliyopo juu yao ikapoteza.

Kushinda kwa Lorient kutakuwa kumewafanya kufikisha pointi 32 sawa na Le Havre lakini wao watakaa juu kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa ikiwa watafunga zaidi ya mabao 11 dhidi ya PSG.

Chanzo: Mwanaspoti