Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fundi mpya aanza tizi Simba

Babacar Sarr. Babacar Sarr.

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mpya wa Simba, Babacar Sarr jana ameanza kazi kujifua na timu hiyo kwenye mazoezi ya timu hiyo yatakayofanyika nje ya Uwanja wa New Amaan Complex.

Sarr ambaye amesajiliwa juzi ataanza mazoezi na kikosi cha timu hiyo yakiwa ndio mazoezi yake ya kwanza na wekundu hao.

Mapema jana kiungo huyo amefanya kikao cha kwanza na kocha wa timu hiyo Abdelhak Benchikha sambamba na kuwasalimia wenzake kwa utambulisho maalum.

Sarr raia wa Senegal ndiyo usajili wa kwanza wa Simba kwenye dirisha dogo la usajili kwa wachezaji wa kigeni yakiwa ni mapendekezo ya kocha Benchikha ambaye alitaka aletewe kiungo mkabaji.

Hata hivyo Sarr hataweza kuwa sehemu ya kikosi cha kesho cha Simba kwenye mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Mapinduzi kocha msaidizi wa Simba Seleman Matola amethibitisha.

"Hataweza kucheza leo ndio kwanza amefika, huko mbele tunaweza kuja kumuona lakini kwa mechi hii atakuwa nje kujifunza kidogo, bado tuna kikosi kipana kitakachoweza kutupa matokeo kwenye mechi ya kesho dhidi ya Jamhuri,"amesema Matola.

Sarr anatua Simba akiwa kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba mfupi na klabu yake ya Saudi Arabia aliyoitumikia mara ya mwisho kabla ya kutua kwa wekundu hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live