Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fundi Balama utamu uko hapa!

Balama+pic Fundi Balama utamu uko hapa!

Thu, 1 Oct 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By CHARITY JAMES HABARI ya mjini kwa sasa ni kuhusu Kariakoo Derby itakayopigwa Oktoba 18 kama haitakumbwa na panguapangua ya ratiba ya Ligi Kuu Bara.

Mashabiki wa Simba na Yanga hawawezi kusahau tukio lile la kupindua meza kibabe lililofanywa na Wanajangwani katika mechi yao ya Januari 4, 2020 baada ya kutanguliwa mapema kwa mabao 2-0.

Simba ilitangulia kwa bao la penalti ya dakika ya 42 lililofungwa na Meddie Kagere ‘MK 14’, ambaye alichezwa faulo na Kelvin Yondani.

Kisha mapema katika dakika ya kwanza ya kipindi cha pili, Simba ikapata bao la pili kupitia kwa Mkongomani Deo Kanda, shukrani kwa asisti tamu ya kisigino ya MK 14.

Kutokana na ubora wa kikosi cha mabingwa watetezi Simba, wengi waliamini siku hiyo Yanga ingeoga mvua ya mabao, hasa kutokana na historia ya wachezaji wa Yanga kuingia maji wanapotanguliwa mabao na Simba.

Lakini alikuwa ni Mapinduzi Balama ‘Kipenseli’ aliyeamsha mizuka ya Yanga kupitia bao lake la shuti la mbali kutokea nje ya boksi, baada ya kumnyang’anya mpira Mzamiru Yassin.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz