Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Frenkie de Jong kufanywa chambo FC Barcelona

De Jong Frankoe.jpeg Frenkie de Jong kufanywa chambo FC Barcelona

Mon, 17 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Mabingwa wa Soka nchini Hispania FC Barcelona Frenkie de Jong, huenda akawa sehemu ya ofa itakayotumwa na klabu hiyo kwenda Manchester City kwa ajili ya kuipata huduma ya Bernardo Silva, katika dirisha hili.

De Jong ambaye amekuwa kuhusishwa na Manchester United tangu dirisha lililopita atajumuishwa kwenye dili hilo ili Barca isilipe pesa kwenye dili la Bernardo Silva.

Barca ilihitaji huduma ya Silva mwenye umri wa miaka 28 tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi lakini dili lilifeli baada ya Man City kugoma kumuuza.

Nyota huyo wa Man City anaonekana kusubiri kwa hamu kubwa Barca iombe kumsajili anaonekana kuwa tayari kuondoka ili kutafuta changamoto mpya mahali pengine kwa kuwa anaona hana alichobakisha kwenye kikosi cha matajiri hao.

Kocha wa Barcelona, Xavi Hernandes amekuwa akimhusudu sana fundi huyu akiamini uwepo wake utasaidia kuboresha eneo lake la kiungo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live