Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Freddy: Tulieni, hapa Simba nitafunga sana!

Freddy Michael Kouablan.jpeg Freddy Michael Kouablan

Fri, 2 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kikosi cha Simba kipo mjini Kigoma tayari kwa pambano la Ligi Kuu Bara litakalopigwa kesho Jumamosi dhidi ya Mashujaa ya Kigoma, huku straika mpya wa timu hiyo Freddy Michael Kouablan, amewatoa hofu mashabiki na viongozi wa klabu hiyo kuwa, wasiwe na hofu naye kwenye ishu ya kufunga mabao.

Freddy amesema linapokuja suala la yeye kuifanya kazi yake ya kutupia nyavuni, hajawahi kukosea katika timu alizotoka, hivyo hata Wanasimba wasiwe na presha naye, kwani atawapa raha.

Raia huyo wa Ivory Coast, amesajiliwa na Simba hivi karibuni kupitia dirisha dogo akitokea Green Eagles ya Zambia akiwa ameichezea mechi 17 msimu huu na kuifungia mabao 14 na kuasisti nne na juzi katika mechi ya Kombe la ASFC, aliasisti bao la kwanza la Simba lililofungwa na Luis Miquissone walipoifumua Tembo F kwa mabao 4-0.

Alizungumza na Mwanaspoti kabla ya kwenda Kigoma kuwahi mechi ya leo la Ligi Kuu Bara dhidi ya Mashujaa, nyota huyo amesema bado anaendelea kuzoea mazingira na maisha mapya ndani ya Simba kabla ya kuanza mambo huku akikiri kwa muda mfupi aliokaa amefurahia mambo mengi.

Amesema amefarijika sana mapokezi aliyopatiwa na wachezaji wenzake na viongozi bila kuwasahau na makocha kwa ujumla.

"Kama kuna kitu sina wasiwasi nacho basi ni juu ya ujuzi wangu wa kufunga na kwa namna nilivyoiona timu hakuna kinachoshindikana kupata mabao kutokana na ubora wa wachezaji nilivyouona," amesema Freddy, huku kocha wa kikosi hicho Abdelhak Benchikha, akisema wachezaji wapya ni mapema kuwapima kwa kutumia mechi moja, akisisitiza bado wana muda wa kufanya vizuri, akiwataka kuzoea haraka mazingira.

"Hatutakuwa na haki kuwapima kwa kuangalia hii mechi Moja ambayo wamecheza, ni mapema kidogo tuwape muda wanatakiwa kuzoea baadhi ya mambo, lakini wanatakiwa kujituma sana," amesema Benchikha na kuongeza; "Changamoto kubwa kwao ni kwamba wamekuja kwenye usajili ambao tayari timu ipo kwenye mashindano na nguvu yao inahitajika pia kubadilisha baadhi ya mambo."

Mchezaji mkongwe wa kikosi hicho, Shomari Kapombe amewazungumzia wachezaji wapya kwa kusema ni wazuri ila kuna kuna jambo moja hawatakiwi kufanyiwa.

"Wachezaji wapya wameonyesha ubora mkubwa hasa mazoezini, lakini kwa sasa hawatakiwi kuwekewa presha kubwa ya kutakiwa kufanya kazi kwa mafanikio."

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: