Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Freddy Michael ametolewa kafara Yanga - mchambuzi

Fred Michael Simba (1) Freddy Michael Kouablan.

Wed, 21 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka East Africa Radio, Samwel Rashid mwenyewe anajiita Wakanda Republic amedai kuwa aliyekuwa mshambuliaji wa Simba SC, Freddy Michael Kouablan ametoa kafara ili kupisha usajili wa mshambuliaji mpya, Leonel Ateba.

Freddy ambaye ni raia wa Ivory Coast tayari ameshaondolewa kikosini hapo na inasemekana ametua USM Alger ya Algeria huku Ateba aliyekuwa USM Alger akitua Simba Sc dakika za mwisho kabisa kabla dirisha la usajili halijafungwa.

"Kuondoka kwa Freddy ni suala ambalo Simba lilikuwa nje ya uwezo wao, Simba walihitaji straika na muda huo huo idadi ya wachezaji wa kigeni ilikuwa imekamilika 12 hivyo Ateba angekuwa wa 13, kwa hiyo ilibidi mmoja atolewe kafara, na mchezaji ambaye huwa anatolewa kafara ni yule ambaye inakuwa rahisi kuachana nae.

"Mezani wachezaji ambao walikuwa rahisi kuachana nao ni Ayoub Lakred pamoja na Freddy, sasa vigezo vya kuvunja mkataba wa Ayoub vilikuwa ni vigumu kiasi kwamba Simba wangetakiwa kumlipa pesa nyingi sana, kwa hiyo kafara ikamuangukia Freddy ambaye yeye mkataba wake ulikuwa ni wa mwaka mmoja na ilikuwa rahisi kuuvunja," amesema Wakanda Republic.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live