Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Freddy Fungafunga awaonya mabeki Ligi Kuu 2024/25

Wanamkosea Fred Easd Freddy Fungafunga awaonya mabeki Ligi Kuu 2024/25

Wed, 10 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabeki wa timu pinzani mmemsikia, Mshambuliaji wa simba, Freddy Michael? mwamba anasema kuwa safari hii amekuja kivingine kusaidia timu yake hiyo inafanya vizuri kwa msimu wa 2024/25.

Akizungumza na Spotileo, Fredy amesema safari hii ameweza kupata muda mzuri wa kufanya maandalizi na timu wakiwa wachezaji wote na kuanza mapema kutengeneza muunganiko na wachezaji wenzake.

Fredy alisajiliwa na Simba kipindi cha dirisha dogo na kufanikiwa kufunga mabao 9 katika mechi za mzungumko wa pili wa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara, Wekundu hao wa Msimbazi wakimaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.

“Hiki ni kipindi kizuri kwangu kwa sababu nitakuwa nimepata muda wa kujiandaa na nitapambana kila mechi kuhakikisha natumia nafasi kusaidia timu  kupata makombe,” amesema Freddy.

Ameongeza kuwa anaimani ya kufanya vizuri na kusaidia timu yake kwa sababu kazi yake kubwa ni kufunga na kusaidia timu hiyo kufikia malengo ya kutafuta matokeo ya ushindi.

Freddy akitokea Green Eagles ya Zambia alijiunga na Simba, Januari na kufanikiwa kutwaa kiatu cha ufungaji bora wa Ligi ya nchini humo (FAZ /MTN Super League), msimu wa 2023/24 akifunga mabao 14.

Kwa kuwa hakuna mshambuliaji mwingine nchini humo alifikia kwenye ligi hiyo aliweza kufikia mabao 14 katika mechi 16 pekee alizofanikiwa kucheza akiwa na Green Eagles kabla ya kujiunga na Simba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live