Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Frank Ribery aanika kustaafu Soka

Reibery Frank Ribery

Fri, 7 Oct 2022 Chanzo: dar24.com

Kiungo wa zamani wa klabu ya Fc Bayern Munich na timu ya taifa ya Ufaransa Frank Ribery amepanga kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 39.

Kiungo huyo ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Salernitana imayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Italia maarufu kama Serie A, amepanga kuvunja mkataba na klabu hiyo ili aweze kustaafu soka baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa mwaka mmoja sasa baada ya kutoka klabu ya Fiorentina inayoshiriki ligi hiyo pia.

Frank Ribery ambaye amepata umaarufu zaidi katika klabu ya Fc Bayern Munich ambapo alicheza kwa mafanikio makubwa akiwa na pacha wake Arjen Robben akipata mafanikio makubwa klabuni hapo, Pamoja na kushinda kila taji kwenye ngazi ya klabu kwa miaka 12 aliyoitumikia miamba hiyo ya soka nchini Ujerumani kabla ya kutimkia klabu ya Fiorentina ya nchini Italia mwaka 2019.

Frank Ribery atakumbukwa zaidi mwaka 2013 ambapo alikua na msimu bora zaidi na kufanikiwa kufanikiwa mchezaji bora ulaya na kushika nafasi ya tatu kwenye tuzo za Ballon dor, Pia alifanikiwa kuisaidia klabu yake kushinda mataji matatu ndani ya msimu mmoja wa 2012/13.

Chanzo: dar24.com