Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Frank Ribéry arejea Bayern

 Frank Ribery.jpeg Frank Ribéry

Thu, 17 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa zamani wa Bayern Munich na Ufaransa, Frank Ribéry anatarajiwa kurejea katika klabu hiyo ya Bundesliga chini ya jukumu jipya.

Ribery (39) anatarajiwa kuwa balozi wa klabu, mazungumzo ya awali tayari yamefanyika kati ya pande zote mbili na yanaendelea vizuri.

Ribéry atachukua majukumu ya uwakilishi (Balozi) wa Bayern katika siku zijazo, si mchezaji wa kwanza wa zamani kuchukua nafasi hii huku wachezaji kama vile Giovane Elber (50) na Claudio Pizarro (44) wakiwa tayari wamechukua kazi sawa na klabu.

Tangu alipostaafu mwezi Oktoba kutokana na majeraha ya mara kwa mara ya goti, Ribéry amekuwa akifanya kazi kama kocha msaidizi katika klabu ya Serie A, Salernitana ambaye kwa sasa ipo nafasi ya 12.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live