Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Frank Leboeuf awapasualia ukwei mashabiki Chelsea

Leabouf Frank Leboeuf awapasualia ukwei mashabiki Chelsea

Fri, 2 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Nyota wa zamani wa Chelsea, Frank Leboeuf amewaambia mashabiki wa Chelsea wanatakiwa kuwa wavumilivu kwani miamba hiyo kusajili wachezaji wengi vijana kwa pesa ndefu si kujenga timu kwa mpango wa baadaye ni wa sasa na kwa maana hiyo kuhusu makombe, watasubiri sana.

Inaelezwa kutokana na usajili unaofanywa na klabu hiyo ya Darajani, Mashabiki wamekuwa na matumaini makubwa ya kubeba taji la Ligi Kuu England, lakini Leboeuf (56) amesisitiza timu hiyo huenda isishinde tena taji la Ligi Kuu England.

Leboeuf amewaambia mashabiki wanahitaji kuvumilia sana katika kipindi hiki kwani mambo hayawezi kuwa sawa kwa muda mfupi ujao kutokana na yale yanayoendelea katika timu na hata mabosi wa timu hiyo kukubali kuvumilia ili timu ijengwe, wanakiona kama fedheha kwao, hivyo hawawezi hata siku moja kuvumilia.

"Baadhi ya mashabiki wanafikiri Chelsea inaweza kukubali kuvumilia kutengeneza timu kuanzia msimu ujao, sio kweli haitoweza kuvumilia kwa sababu imeshatumia pesa nyingi katika usajili. Chelsea ya sasa inaweza kufanya chochote inachotaka kwa kutumia pesa zao, lakini sisi kama wachezaji wa zamani, nadhani naona aibu kwa kile tunachokiona. Kuna wachezaji wengi wenye vipaji katika kikosi lakini hakuna wachezaji viongozi au wale wenye uzoefu unaoweza kuwategemea, nafikiri hilo ndio tatizo kubwa analokumbana nalo Enzo Maresca."

Miamba hiyo ambayo ikiwa chini ya mmiliki Roman Abramovich ilikuwa na mafanikio makubwa karibia katika kipindi chake chote, mambo yamekuwa magumu chini ya mmiliki mpya, Tody Boehly tangu alipoichukua mwaka 2022 na imetumia kiasi kikubwa cha fedha kusajili mastaa mbalimbali.

Leboeuf aliongeza; "Inawezekana Chelsea inaweza kushinda kombe kama vile FA msimu huu, lakini sio Ligi Kuu England, haiwezekani. Kama wataendelea kusajili wachezaji wa aina hii pekee, hawatoshinda tena Ligi Kuu, wanahitaji wachezaji wenye uzoefu," alisema lejendari huyo.

"Wakati najiunga na timu wakati huo niliikuta haijashinda Ligi Kuu kwa miaka 26, lakini jambo hilo liliwezekana muda mfupi tu baada ya wachezaji bora na wenye uzoefu waliposajiliwa katika timu."

Baadhi ya mashabiki wa timu hii pia wanaonyesha kutofurahishwa na maendeleo ya timu yao na sera ya usajili kwa jumla.

Moja ya mambo yanayowakera ni jinsi utawala huo mpya usivyowapa nafasi wachezaji waliolelewa na Chelsea kuanzia kwa Trevoh Chalobah ambaye hakujumuishwa katika kikosi kilichopo Marekani kwa ajili ya maandalizi ya msimu pamoja na Conor Gallagher amewekwa kwenye mpango wa kuuzwa tangu msimu uliopita.

Kundi la 'The Chelsea Supporters Trust' inadaiwa limeiandikia barua timu hiyo kutakuwa na ongezeko kubwa la maandamano kupinga namna Boehly na watu wake wanavyoiongoza timu hiyo.

Chanzo: Mwanaspoti