Frank Lampard mbioni kutangazwa kama kocha mkuu wa timu ya Norwich City muda wowote kuanzia sasa kutokana na uhitaji mkubwa wa kocha kwenye klabu hiyo tokea imuoneshee njia ya kutokea Daniel Farke.
Frank Lampard kocha wa zamani wa vilabu vya Derby na Chelsea anatarajia kubeba majukumu ya Daniel Farke, ambaye alifutwa kazi wiki iliyopita baada ya kupata ushindi wake wa kwanza dhidi ya Brentford. Frank Lampard
Lampard amekuwa hana kazi tokea alipofungashiwa virago na klbau ya Chelsea mwezi januari baada ya kuwa na matokeo mabovu, na kutoka kwenye nafasi nne za juu mpaka nafasi ya tisa.
Kwasasa Lampard anajianda kubeba mzigo uliomshinda Daniel Farke kuitoa Norwich City kutoka kwenye hatari ya kushuka daraja na kurudisha hamasa ya ushindi kwa wachezaji na klabu nzima kwa ujumla.