Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Frank Lampard amkingia Kifua Dele Alli

Lampard Frankk Frank Lampard

Tue, 8 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa timu ya Everton Frank Lampard amemkingia kifua mchezaji wake mpya baada ya Glenn Hoddle kukosoa mavazi yake kwenye mchezo wa wikiendi alipohudhuria mchezo dhidi ya Brentford.

Alli na Donny van de Beek walitambulishwa kwenye uwanjwa wa nyumbani kwenye kipindi cha kwanza kwenye mchezo wa FA Cup raundi ya nne ambao Everton walishinda kwa goli 4-1 dhidi ya Brentford.

Mchezaji wa zamani wa Tottenham Hoddle alimkosoa Dele Alli baada kusimama mbele ya umati wa mashabiki wa klabu ya Everton na kusema kuwa allli alikuwa kama mtu aliyeokotwa tu mtaani.

Frank Lampard alipozungumza na waandishi wa habari kabla ya mchezo wao na Newcastle kesho jumanne, alinukuliwa akisema, “sijari gari gani anaendesha, nguo gani anavaa ilimradi naweza kuwa nae kila siku mazoezini, na anahitaji kuwa bora kila siku, anaheshimu klabu na anawaheshimu wachezaji wanzake.

“Mpira wa kisasa umebadilika sana wote tunapaswa kutambua hilo, simjibu mtu kwa sababu ya mtamzamo wake, kila mmoja anaruhusiwa kuwa na mtazamo wake binafsi lakini naweza kupambana na vitu vilivyo mbele yangu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live