Kiungo wa Al-Ahli Saudi FC ya Saudi Arabia, Franck Yannick Kessié amefunguka sababu ya staili yake ya kushangilia kwa kupiga salute.
Frank ambaye amewahi kutumikia AC Millan ya Italy na Barcelona ya Hispania, alifunga bao moja kati ya mawili waliofunga Ivory Coast kwenye fainali ya AFCON 2023 na kufanikiwa kuchukua ndoo hiyo.
“Baba yangu alikuwa ni mchezaji mpira wa miguu Ivory Coast, lakini mwishowe aliishia kuwa mwana-jeshi na kuitumikia nchi yake. Alifariki kutokana na maradhi wakati huo nikiwa na miaka 11.
“Pindi ninapo funga goli, napenda kushangilia kwa salamu ya kuweka saluti ili kumpa heshima baba yangu,” amesema Franck Kessie.