Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Francesco Totti amkingia kifua Mourinho

Jose Mourinho Roma Kocha wa AS Roma, Jose Mourinho

Sun, 14 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jose Mourinho siyo tatizo kwenye klabu ya AS Roma, na klabu na mashabiki kwa pamoja wanapaswa kumuunga mkono. Kwa mujibu wa Francesco Totti.

Roma walimteua Mourinho kuwa meneja mwezi Mei, na waliwekeza takribani Euro milioni 130 kwa ajili ya wachezaji wapya.

Licha ya mambo kuanza vyema, Roma wakishinda mechi zao sita za msimu kwa mara ya tatu kwenye historia yao, wameshinda mechi nne pekee katika mechi 12 walizocheza ugenini.

Baada ya hapo fomu ya Roma ikaanza kuporomoka na wakimaliza safari yao ya ushindi wa mechi 43 mfululizo za nyumbani .Mwezi Novemba pia haujawa mwema sana kwa Roma wakianza na kutoa sare nyumbani dhidi ya Bodo, kabla ya kukubali kichapo cha 3-2 dhidi ya Venezia.

“Kama tukidhani tatizo la Roma ni Mourinho, inamaanisha kila kitu hakiko sawa kwetu. Saluti kwa Mourinho, ameshinda mechi nyingi zaidi ukifananisha na mameneja wengine wote wa Serie A. Klabu na mashabiki wanapaswa kumuunga mkono"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live