Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fountain yaendeleza uteja kwa Simba Queens

Simba Queens 2 1 Fountain yaendeleza uteja kwa Simba Queens

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) kati ya Fountain Gate Princess dhidi ya Simba Queens umemalizika katika uwanja wa Jamhuri jijini hapa kwa wenyeji kuendeleza uteja kwa kukubali kichapo cha mabao 2-1.

Mabao ya Simba Queens yamefungwa na Mkenya Jentrix Shikangwa na Ruth Ingosi dakika za 70 na 87 huku lile la Fountain likifungwa na Neema Paul.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza Simba Queens waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

ZIFUATAZO NI DONDOO MUHIMU ZA MCHEZO HUU

Katika michezo minne iliyokutana timu hizo katika Ligi, yote Simba Queens imeibuka na ushindi.

Huu unakuwa mchezo wa pili kwa Fountain Gate kupoteza msimu huu ikiwa imeshinda michezo tisa(9).

Huu ni ushindi wa tisa (9) kwa Simba Queens huku ikiwa imepoteza mchezo mmoja pekee

Matokeo haya yanaishusha Fountain hadi nafasi ya tatu ikiwa na pointi 29 huku JKT Queens ikiongoza Ligi kwa kuwa na pointi 31, ikifuatiwa na Simba Queens yenye pointi 30

Bao la Neema Paul la tano (5)kwake msimu huu huku kinara katika timu hiyo kwa ufungaji akiwa ni Cynthia Musungu mwenye mabao tisa (9)

Nyota wa Simba Queens mkenya Jentrix Shikangwa hilo ni bao lake la 11 msimu huu na anakuwa kinara wa mabao katika Ligi hiyo.

Kipa wa Simba Queens,Caroline Rufa ambaye alianza katika mchezo wa leo, msimu uliopita aliichezea Fountain Gate Princess na kuisaidia kumaliza kwenye nafasi ya pili huku Simba Queens wakichukua ubingwa.

Chanzo: Mwanaspoti