Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fountain Gate yanunua Uwanja wa Gwambina Complex

Gwambina Complex.jpeg Fountain Gate yanunua Uwanja wa Gwambina Complex

Sat, 11 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya Fountain Academy imeununua uwanja wa Gwambina Complex uliopo wilayani Misungwi katika Jiji la Mwanza ambao ulikuwa ukitumiwa na timu ya Gwambina FC, na sasa uwanja huo utatambulika kwa jina la Fountain Gate Stadium Mwanza.

Uwanja huo Kwa Sasa unafahamika kama Fountain Gate Studium huku ukilenga kutumia katika Programu za Michezo za Watoto wa kike GETS Program (Girls Empowerment Through Soccer) na zile za Watoto wa kiume za YETS ( Youth Empowerment Through Soccer) Kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa.

Zoezi la kununuliwa kwa Uwanja huo linaambatana na zoezi la kuinunua Shule ya Sekondari ya Elpas ya wilayani Misungwi mkoani Mwanza ambapo hivi sasa inatambulika kama Shule ya Sekondari Fountain Gate Mwanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live