Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fountain Gate yakamilisha usajili wa Husna Mpaja

Xvdf Husna Fountain Gate yakamilisha usajili wa Husna Mpaja

Thu, 7 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Fountain Gate Princess imekamilisha usajili wa mshambuliaji Husna Mpaja kutokea Klabu ya Makerere University inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uganda.

Husna mpaja ni Mtanzania mzaliwa wa Bukoba anajiunga na Fountain Gate baada kufanya vizuri kunako Uganda ambako ametumika kwa nusu msimu tu huku rekodi zake zikiwa.

Mechi - 07

Magoli - 05

Asisti - 03

Husna amewahi kuhudumu kunako Ruvuma Queens kisha baadaye Tiger Girls ambako alikuwa kapteni na aliwasaidia kupanda daraja kabla ya hapo baadaye kuamua kutimkia nchini Uganda.

Mchezaji huyo ana mudu kucheza nyingi uwanjani mshambuliaji, Beki wa kati au kiungo (Mshambuliaji/Mzuiaji).

Yanga Princess walikuwa katika hatua nzuri zaidi kumchukua kabla ya Fountain Gate Princess kupita mlango wa nyuma na kuinasa saini yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live