Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fountain Gate yaiandalia kiama Simba Queens

Fountain Gate Princesss Fountain Gate yaiandalia kiama Simba Queens

Fri, 30 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Achana na ushindi wa mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) Fountain Gate Princess (FGP) inapiga tizi la kufa mtu kuhakikisha inapata matokeo mazuri katika mchezo wao ujao dhidi ya Simba Queens unaotarajia kuchezwa Januari 4, mwakani kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena.

Msimu uliopita Simba Queens ilitwaa ubingwa wa ligi hiyo ikishinda michezo yote iliyocheza huku Fountain Gate Princess ikishika nafasi ya pili.

Simba ilishinda nyumbani mabao 3-1 kisha ikaibuka na ushindi mzito ugenini Uwanja wa Fountain Gate Arena mkoani hapa kwa mabao 4-0, huku pia Simba Queens ikishinda mabao 2-0 katika mechi ya Simba Day iliyochezwa Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Kocha wa timu hiyo, Alex Alumirah alisema wanaendelea na mazoezi makali kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo ambao anaamini utakuwa mkali na wa kusisimua.

“Nazitaka sana pointi za Simba ndio maana haya mapumziko ya wiki mbili tunaendelea na mazoezi, lakini kila mechi kwetu ni muhimu,” alisema kocha huyo ambaye pia huifundisha wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Kenya

Chanzo: Mwanaspoti