Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fountain Gate kutema 13

Fountain Gate Champ Fountain Gate kutema 13

Tue, 13 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Fountain Gate Fc,inayoshiriki Championship Furgence Novatus ametangaza kuwaacha nyota 13 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo majeruhi, uwezo mdogo na nidhamu.

Fountain kwenye Championship msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya saba ikiwa na pointi 43 huku timu za JKT Tanzania na Kitayose zikipanda moja kwa moja kucheza ligi kuu.

Kocha huyo ambaye amewahi kuzinoa timu za Gwambina na timu za taifa ya Bara, Kilimanjaro Stars, alisema wameamua kuwaacha wachezaji hao kutokana na kushuka uwezo,majeruhi ya mara kwa mara,pamoja na nidhamu.

Alisema msimu ujao wamepanga kuwa na wachezaji 25 pekee hivyo wataongeza wachezaji sita kutokana na mapungufu ya msimu uliopita.

“Tutaweka wazi tuliowaacha lakini tulikuwa na changamoto ya nidhamu,majeruhi pamoja na baadhi kuwa na uwezo mdogo,malengo yetu msimu ujao ni kucheza ligi Kuu,”alisema kocha huyo.

Alisema kikosi cha timu hiyo kinatarajia kuingia kambini Julai mosi mwaka huu wilayani Gairo kwa ajili ya kuajiandaa na ligi hiyo na maandalizi ya msimu.

“Safari hii tutawapa nafasi zaidi wachezaji vijana, kwa sasa tupo katika kutafuta vipaji kwa ajili ya timu yetu ya vijana na baadhi tutaongeza katika timu ya wakubwa ili kuweka mambo yakae sawa kwa sababu soka linachezwa na vijana,” alisema kocha huyo.

Mkurugenzi wa Fountain Gate School, Japhet Makau alisema watasajili wachezaji wenye uwezo kwa mapendekezo ya benchi la ufundi linaloongozwa na Novatus.

Novatus alichukua nafasi ya kocha raia wa Uganda Kefa Kisala ambaye uongozi wa Fountain uliamua kumtupia virago kutokana na matokeo mabovu ya timu hiyo katikati ya msimu uliopita.

Chanzo: Mwanaspoti