Uongozi wa Fountain Gate Princess umeweka wazi kuwa wamepata fursa nyingine kwa tmu hiyo kushiriki kwenye Ngao ya Jamii kwa Wanawake.
Taarifa iliyotolewa imeeleza namna hii:”Tunapenda kuwafahamisha rasmi kuwa Timu yetu ya Wanawake Fountain Gate Princess inatarajia kushiriki Ngao ya Jamii Kwa Wanawake ambayo ni ishara ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi ya Wanawake Tanzania.
“Ikiwa ni kwa mara ya kwanza kufanyika, Ngao ya Jamii itakutanisha jumla ya timu nne za wanawake (JKT Queens, Simba Queens, Fountain Gate Princess na Yanga Princess) na mechi hizi zitachezwa Jijini Dar es Salaam kama ratiba ilivyoambatishwa hapo.
“Mdhamini wa Shindano hili ni Vodacom Tanzania na wanatoa zawadi kama ifuatavyo: Bingwa – 5M, Mshindi wa Pili – 3.5M, Mshindi wa tatu – 1.5 M na mshindi wa nne – 1M.
“Timu yetu tayari ipo jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wake ambapo tumepangwa kucheza dhidi ya JKT Queens. Michezo hii itakuwa Mubashara kupitia Azam TV. Kwa mara nyingine tena ni fursa adhimu kwetu kuitangaza na kuipeleka nembo yetu,” Ofisa Habari wa Singida Fountain Gate, Hussein Masanza.