Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Forbes yaanika wachezaji wanaoingiza pesa nyingi zaidi

Mbappe Ronaldo Messi Forbes yaanika wachezaji wanaoingiza pesa nyingi zaidi

Wed, 26 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jarida maarufu la Forbes limemtaja Kylian Mbappe, 23 kuwa ndiye mwanasoka anayeingiza pesa kubwa zaidi duniani kwa sasa ikiwa ni mara ya kwanza kwa mchezaji mbali na Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ambao wamekuwa nakuwa katika kipindi cha miaka tisa.

Forbes inakadiria kuwa Mbappe ambaye ni mshambuliaji wa Paris Saint-Germain (PSG) atatia mfukoni kima cha Sh15.6 bilioni msimu huu.

Messi anayeshirikiana na Mbappe pamoja na Neymar Jr katika safu ya mbele ya PSG ni wa pili kwa kima cha Sh14.6 bilioni huku wakisogelewa kwa karibu na Ronaldo anayetandazia Manchester United (Sh12.2 bilioni).

Neymar na mfumaji matata wa Liverpool, Mohamed Salah, wanafunga orodha ya tano-bora kwa Sh10.6 bilioni na Sh6.5 bilioni.

Erling Haaland wa Manchester City anakamata nafasi ya sita (Sh4.8) bilioni mbele ya Robert Lewandowski (Barcelona), Eden Hazard (Real), Andreas Iniesta (Vissel Kobe) na Kevin de Bruyne (Man-City).

Mchezaji wa mwisho kuwahi kuongoza orodha hiyo mbali na Ronaldo na Messi ni nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, David Beckham mnamo 2013.

Mbappe alitia saini mkataba mpya wa miaka mitatu kwa ahadi ya mshahara mkubwa kambini mwa PSG mnamo Mei na kukomesha tetesi za kujiunga kwake na Real Madrid.

Nyota huyo aliyesaidia Ufaransa kuzoa Kombe la Dunia mnamo 2018, amenyanyulia PSG mataji 11, yakiwemo 11 ya Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1), tangu aagane na AS Monaco mnamo 2017.

Mbappe na Haaland ndio wanasoka wa pekee chini ya umri wa miaka 30 katika orodha hiyo ya 10-bora ya Forbes.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live