Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fofana avunja ukimya sakata la ubaguzi la Enzo Fernandez

Enzo Fernandez And Wesley Fofana Fofana avunja ukimya sakata la ubaguzi la Enzo Fernandez

Fri, 2 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa Chelsea, Wesley Fofana amevunja ukimya kuhusu sakata la ubaguzi wa rangi la kiungo Enzo Fernandez na kubainisha kuwa Muargentina huyo sio mbaguzi baada ya kuwaomba msamaha wachezaji wenzake wa Chelsea.

Mapema mwezi huu Enzo akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa alionekana kwenye video iliyovuma kwenye mitandao ya kijamii akiimba nyimbo za kibaguzi kuhusu wachezaji wa Ufaransa wenye asili ya Kiafrika hali iliyozua taharuki miongoni mwa wachezaji wa klabu hiyo.

Fofana ambaye pia ni Mfaransa amezungumzia tukio hilo hadharani kwa mara ya kwanza na kufunguka jinsi yeye na wachezaji wengine walivyojisikia ambapo alielezea wimbo huo kama “ubaguzi wa rangi usiozuiliwa”.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live