Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Foden amvutia fundi wa usajili Madrid

Phil Foden Contract Phil Foden

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mkuu wa kitengo cha kusaka vipaji wa klabu ya Real Madrid ameripotiwa kuvutiwa na huduma ya kiungo Phil Foden baada ya kuonyesha kiwango bora sana kwenye kikosi cha Manchester City.

Kiungo huyo alikuwa steringi wa mchezo wakati Man City ilipoichapa Manchester United kwenye kipute cha Manchester derby, Jumapili iliyopita.

Katika mechi hiyo, Foden alifunga mara mbili Man City ilipotokea nyuma na kushinda 3-1 uwanjani Etihad. Kwa mujibu wa ripoti za kutoka Hispania, skauti mkuu wa Real Madrid, Juni Calafat alivutiwa na huduma ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23.

Bosi huyo wa wasaka vipaji wa Los Blancos anaamini Foden anaweza kwenda kuongeza kitu kikubwa kwenye kikosi chao huko Bernabeu, likibainisha Defensa Central.

Kinachoelezwa ni Calafat ndiye silaha ya siri ya Real Madrid katika kunasa mastaa wapya kwenye kikosi hicho na kuwafanya kuwa imara zaidi ndani ya uwanja.

Foden amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu akifunga mabao 18 katika michuano yote na kuasisti mara saba, lakini kwenye Ligi Kuu England amefunga mabao 11 na asisti saba. Mkataba wake umebakiza miaka mitatu baada ya kusaini dili jipya Oktoba 2022.

MKALI FODEN KWENYE EPL MSIMU HUU

-Amecheza: Mechi 27

-Ametengeneza: Nafasi 57

-Amepiga: Pasi 1,301

-Amefunga: Mabao 11

-Ametoa: Asisti 7

Chanzo: Mwanaspoti