Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Foden alivyowavuruga Arsenal kwa sekunde 60

Foden Phillll Foden alivyowavuruga Arsenal kwa sekunde 60

Mon, 20 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Hali ya mashabiki wa Arsenal iliyokuwa kwenye majonzi na masikitiko makubwa ndani ya sekunde 60 za mchezo wao wa kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England dhidi ya Everton jana Jumapili.

Ikiwa Emirates, mashabiki wa Arsenal masikio yao yote yalielekezwa huko Etihad, ambako wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa huo, Manchester City ilikuwa ikikipiga na West Ham United na kila kitu kilikuwa kimetibuka kwa The Gunners baada ya vijana wa Pep Guardiola kufunga bao la kuongoza kwenye sekunde ya 79 tu ya mchezo.

Ili kubeba taji la Ligi Kuu England msimu huu, kikosi hicho cha kocha Mikel Arteta kilihitaji West Ham iichape Man City, huku wao wakihakikisha wanawachapa Everton.

Lakini, ndoto zao hizo zilizimwa mapema sana baada ya Man City kufunga haraka sana bao lao la kwanza kwa muda usiozidi dakika mbili.

Phil Foden alipofunga bao hilo huko Etihad, simanzi kubwa ilihamia Emirates, ambapo picha ziliwaonyesha mashabiki wa Arsenal wakishika vichwa vyao.

Bao hilo la Man City liliwanyong’oneza sana mashabiki wa Arsenal na kuana kuona mapema dalili za kukosa ubingwa huo, ambapo kwa sasa imeshapita miaka 20 bila ya taji la Ligi Kuu England.

Baada ya hapo, mashabiki walivamia kwenye mitandao ya kijamii na kutoa maoni yao, ambapo mmoja aliandika: “Msijali Arsenal.”

Mwin-gine aliongeza: “Sijawahi kumpenda Phil Foden.”

Shabiki wa tatu, alisema: “Tutajaribu tena msimu ujao.”

Shabiki mwingine aliongeza: “Foden anajitafutia matatizo.”

Mambo yalikuwa mabaya zaidi kwa Arsenal, baada ya Foden kuongeza bao la pili kwenye dakika ya 18 tu.

Na shughuli ya Emirates ilitibuka zaidi baada ya Everton kufunga bao la kuongoza huko Emirates, ambapo mpira wa adhabu wa Idrissa Gueye ulimbabatiza Declan Rice na kutinga nyavuni kwenye dakika 40.

Bao hilo liliwafanya mashabiki wa Arsenal baadhi yao kutoka uwanjani mapema, ambapo kuna wengine walikosa tukio la Takehiro Tomiyasu kusawazisha na kufanya ubao wa matokeo kusomeka 1-1.

Baadaye, walipata matumaini baada ya kusikia taarifa za huko Etihad, kwamba West Ham United imefunga bao kupitia kwa Mohammed Kudus, waliamini kwamba mambo yanaweza kunoga kwamba yakatokea matokeo ya sare kwenye mechi hiyo.

Arsenal ilipambana na kufunga mabao 2-1, shukrani kwa bao la utata la Kai Havertz kwenye dakika 89, lakini ushindi huo haukusaidia kitu, kwamba Man City yenyewe iliongeza bao la tatu na kushinda 3-1 na kunyakua taji lao la nne mfululizo la Ligi Kuu England.

Chanzo: Mwanaspoti