Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Foba aachiwa msala Azam

Dg Zuberi Foba Foba aachiwa msala Azam

Fri, 15 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makipa wa Azam FC, Ali Ahmada na Idrisu Abdulah wapo Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa majeraha yanayo wasumbua.

Ahmada ameondoka nchini usiku wa kuamkia leo Ijumaa kwa matibabu ya goti la mguu wa kushoto, majeraha aliyopata katika mchezo dhidi ya KMC iliyoshinda kwa mabao 5-0.

Idrisu aliondoka Alhamisi akiwa anasumbuliwa na bega la kushoto na wote watafanyiwa matibabu katika Hospitali ya Vincent Palloti, jijini Cape town.

Azam itaongozwa na makipa wawili ambao ni Zuberi Foba aliyecheza mara ya mwisho mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga na kuruhusu mabao mawili kwenye kipigo cha 2-0 na Yassin Hamiss aliyepandishwa kutoka timu ya vijana baada ya Wilbol Maseke kwenda KMC hadi pale watakapo rejea Ali na Idrisu.

Kabla ya kwenda katika mashindano ya Mapinduzi Cup, Azam itacheza michezo miwili, dhidi ya Kagera Sugar ugenini ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara, Desemba 21 na wa FA dhidi ya Alliance uwanja wa nyumbani, Azam Complex, Chamazi, Desemba 17, 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live