Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Flick hakijaeleweka Barca

Kuwasili Kwa Hansi Flick Barcelona Kumecheleweshwa, Sababu Zatajwa.jpeg Hansi Flick

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya kutajwa kuwa kocha mpya wa Barcelona, Hansi Flick bado hajaorodheshwa rasmi kwenye Ligi Kuu Hispania kama bosi mpya huko Nou Camp.

Flick, 59, alitangazwa Mei 29 kuwa ndiye mrithi wa Xavi Hernandez kwenye kikosi hicho cha Nou Camp, ambapo atakuwa Mjerumani wa tatu kuingia kwenye rekodi za kuinoa miamba hiyo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa MARCA, Barca ipo kwenye matatizo makubwa ya kiuchumi, hivyo bado hawajawasilisha baadhi ya nyakara kwenye ofisi za La Liga ili kocha Flick atambulike rasmi.

Na hilo limekwama kutokana na ukomo wa bili ya mishahara ya klabu hiyo kwa sasa. Kinachoelezwa ni kwamba Barca imeshafikia kiwango cha mwisho, hivyo haitaweza kumworodhesha Flick huko La Liga, huku kuna wachezaji wanne pia hawajaorodheshwa kwenye kikosi kwa ajili ya msimu wa 2024/25.

Miongoni mwa wachezaji hao, wamo mastaa wanaochipukia kwa kasi kwenye klabu hiyo, ambao ni kiungo Gavi na beki wa kushoto Alejandro Balde.

Katika kuweka mambo sawa, Barcelona italazimika kukutana na wachezaji wenye mishahara mikubwa kwenye kikosi hicho, kuwashawishi wapunguze mishahara yao ili kuweka sawa bajeti.

Na kuna wachezaji watalazimika kuuzwa kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi, ambapo miongoni mwa wanaotajwa kuwa watafunguliwa mlango wa kutokea ni Eric Garcia, Joao Felix na Joao Cancelo.

Beki wa kati Inigo Martinez naye atapigwa bei kwenye dirisha hili ili kupunguza matumizi.

Chanzo: Mwanaspoti