Timu ya taifa ya Ujerumani imeibuka na ushindi wa 9-0 dhidi ya Liechtenstein katika mchezo wa Kundi J kufuzu Kombe la Dunia barani Ulaya usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Volkswagen Arena Jijini Wolfsburg.
Thomas Muller na Leroy Sane kila mmoja alifunga mabao mawili, wakati mabao mengine yamefungwa na Ilkay Gundogan kwa penalti, Daniel Kaufmann na Maximilian Göppel waliojifunga, Marco Reus na Ridle Baku.
Wageni walilazimika kucheza 10 tangu dakika ya tisa baada ya Jens Hofer kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Leon Goretzka.
Tayari Ujerumani imefuzu fainali zijazo za Kombe la Dunia Qatar ikiongoza Kundi J kwa pointi zake 24, tisa zaidi ya Macedonia Kaskazini wanaofuatia.
Hansi Flick, Kocha wa Ujerumani amekuwa kocha wa kwanza kuiongoza Ujerumani kushinda mechi zake sita za kwanza baada ya ushindi huo wa jana dhidi ya Liechtenstein wa magoli 9-0.