STAA wa zamani kwenye Ligi Kuu ya Italia (Serie A), Francesco Flachi, amerejea kwenye soka akiwa na miaka 46, akicheza ligi ya ngazi ya tano Italia baada ya kumaliza kutumikia kifungo chake cha miaka 12 alichopewa kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya aina ya cocaine.
STAA wa zamani kwenye Ligi Kuu ya Italia (Serie A), Francesco Flachi, amerejea kwenye soka akiwa na miaka 46, akicheza ligi ya ngazi ya tano Italia baada ya kumaliza kutumikia kifungo chake cha miaka 12 alichopewa kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya aina ya cocaine. Straika huyo alizichezea timu kama Fiorentina na Sampdoria, amerejea tangu afungiwe mwaka 2010, na sasa anaichezea Signa 1914. Alicheza wikiendi iliyopita katika sare ya 2-2 dhidi ya Prato 2000.