Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fitna za Pep Guardiola zilivyomng'oa Jesus Man City

Pep X Jesus Fitna za Pep Guardiola zilivyomng'oa Jesus Man City

Mon, 18 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dunia ya mpira ilishuhudia tu Mshambuliaji Gabriel Jesus ametua Arsenal akitokea Manchester City mwaka 2022. Sababu ya kuondoka City haikuelezwa lakini leo imefahamika.

Kwenye mahojiano na Podcast ya The Denilson Show, Gabriel Jesus amefunga yote ambayo yalimchafua roho na kuamua kuikacha Manchester City ambayo aliitumikia kwa miaka mitano.

Jesus anamtaja Kocha Pep Guardiola kuwa chanzo, ambapo anaitaja siku aliyopigwa benchi na nafasi yake alianza Zinchenko.

“Kulikuwa na mechi ya Champions League dhidi ya PSG, nyumbani ambapo alimuanzisha Oleksandr Zinchenko kama namba 9 ya uwongo (false 9). Kitu cha ajabu kweli. Siku moja kabla, hata hakumtumia (Zinchenko) kwenye mazoezi, aliniweka mimi kama Mshambuliaji.

Zinchenko hadi alinitania akisema ‘ile siku nilijisikia vibaya sana juu yako.’ Masaa mawili kabla ya mechi, kulikuwa na Team Talk, wachezaji ilipata chakula na kupumzika kwa dakika 30 na kisha kuingia kwenye mechi.

Hata sikula, nilienda moja kwa moja kwenye chumba na kuangua kilio. Nilimpigia Mama yangu na kumwambia kuwa nataka kuondoka, narudi nyumbani. Kwa sababu alimuingiza Zinchenko. Alimuweka beki wa pembeni kwenye nafasi yangu. Nilipata uchizi.” amesema Gabriel Jesus.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live