By Clezencia TryphoneMore by this Author MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Fiston Abdul Razaq ameliamsha mapema Jangwani kwa kuwatoa hofu mashabiki kwa kuwaambia wakae mkao wa kula kupata mambo mazuri, kwani hajaja kuuza sura Tanzania.
Nyota huyo kutoka Burundi aliwataka wanayanga kukaa mkao wa kula kupata mambo mazuri kutoka kwake akidai wataanza na ubingwa wa Ligi Kuu unaoshikiliwa na watani wao Simba.
Straika aliyesajiliwa katika dirisha dogo lililofungwa katikati ya Januari, alipokelewa juzi na akizungumza na Mwanaspoti alisema anajua kilichomleta nchini na kiu ya mashabiki wa Yanga.
Fiston alisema kazi iliyomleta ndani ya timu hiyo ni moja tu, kuipa timu hiyo mataji ambayo yanawania hivi sasa na kuwashukuru mashabiki walijitokeza na kumlaki Uwanja wa Ndege.
“Nitahakikisha najituma kadri ya uwezo wangu na nawahaidi sana Yanga, nitahakikisha nafunga, ili tutimize malengo yetu,” alisema na kuongeza.
“Tegemeeni mazuri kutoka kwangu mambo mengi tumwachie Mungu sitawaangusha, Daima Mbele, Nyuma Mwiko,” alisema.