Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fiston Mayele aanza kuzungumzwa Tunisia

Mayele 1 Fiston Mayele aanza kuzungumzwa Tunisia

Wed, 19 Oct 2022 Chanzo: Dar24

Baada ya Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ kupanga Droo ya Michezo ya Mtoano ya Kombe la Shirkisho jana Jumanne (Oktoba 18), baadhi ya mashabiki wa Club Africain ya Tunisia wameonesha hofa yao kwa Mshambuliaji wa Young Africans Fiston Kalala Mayele.

Kupitia maoni (comment) katika ukurasa wa timu hiyo baadhi ya mashabiki wameonesha hofu yao kwa Mshambuliaji huyo kwa kuandika ni mchezaji hatari na wa kuchugwa sana, kuelekea mchezo wa Mkondo wa Kwanza ambao umepangwa kupigwa Jumatano (Novemba 02) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

“Nguvu ya timu ya Tanzania (Yanga SC) ipo kwa mshambuliaji wa Congo, Kalala Mayele tu. Mshambuliaji huyu anatakiwa kuchugwa sana na akidhibitiwa hakuna hofu kwa klabu yetu ( Club Africain)” ameandika shabiki mmoja wa Club Africain

Mashabiki hao wameendelea kuichambua Young Africans na kusema kuwa ni timu yenye wachezaji bora wenye nguvu na kasi, hivyo sio ya kuidharau kuwa wataifunga kwa urahisi kama ilivyokuwa kwa timu ya Kipanga ya Zanzibar walioifunga bao 7-0.

Fiston Mayele alimaliza hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na mabao 7 katika michezo 4. Mabao 6 kati ya hayo alifunga dhidi ya Zalan FC, huku bao moja akilifunga dhidi ya Al Hilal ya Sudan.

Chanzo: Dar24