Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fiston Mayele: Ni heshima kubwa kucheza timu ya Taifa

Mayele 763318 Fiston Mayele

Sun, 26 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mara baada ya kufanikiwa kupata nafasi ya kucheza dakika tatu za mwisho katika kikosi cha Timu ya Taifa ya DR Congo, Fiston Mayele ameelezea furaha yake, huku akisema tukio hilo limempa nguvu mpya ya kupambana.

DR Congo katika mchezo wa juzi Ijumaa wa kufuzu AFCON, ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mauritania, mechi ikichezwa Uwanja wa TP Mazembe, Lumbumbashi, DR Congo. Mayele aliingia dakika ya 87 akichukua nafasi ya Cedric Bakambu.

Akizungumza nasi, Mayele alisema: “Ni tukio kubwa sana katika maisha yangu ya mpira kuichezea timu ya taifa ya DR Congo, hii ilikuwa ni ndoto kubwa sana kwangu na nashukuru imetimia, hii imeniongezea pia nguvu ya kuendelea kupambana ili nipate kuitwa mara kwa mara.

“Najua sio kazi rahisi kuitwa mara kwa mara katika timu ya taifa kutokana na ubora wa wachezaji waliopo katika nafasi yangu, lakini lazima nitahakikisha napambana ndani ya timu yangu, naamini nitafanikiwa.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live