Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Firmino hana furaha Saudia, vigogo England kumrudisha

Firmino Spl Firmino hana furaha Saudia, vigogo England kumrudisha

Tue, 2 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Straika wa Al-Ahli, Roberto Firmino yupo kwenye rada za baadhi ya timu za Ligi Kuu England zinazohitaji kumsajili kwenye dirisha hili.

Hii ni baada ya nyota huyo wa kimataifa wa Brazil kudaiwa hana furaha ya kuendelea kuwepo kwenye timu hiyo kutokana na kiwango cha miamba hiyo ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia.

Miongoni mwa timu zinazohusishwa kumsajili staa huyu ni Sheffield United na Everton, lakini changamoto kubwa inaonekana kwenye mshahara wake na inaonekana itakuwa ngumu kwa timu hizo kumlipa.

Hata hivyo, hadi sasa haijawekwa wazi ikiwa Firmino mwenyewe atakubali kuondoka Saudia na kurudi England katika dili litakalopunguza mshahara wake anaoupata sasa.

Firmino ambaye amejiunga na Al-Ahli dirisha lililopita, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2026, kwenye mechi 19 msimu huu amefunga mabao matatu na kutoa asisti tatu.

Chanzo: Mwanaspoti