Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Firmino ainusuru Liverpool na kichapo Anfield

IMG 4117.jpeg Mchezo ulimalizika kwa sare ya mabao 1-1

Sun, 21 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Liverpool wameambulia sare ya kufungana bao 1-1 na Aston Villa katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Jumamosi Uwanja wa Anfield, Liverpool.

Jacob Ramsey alianza kuifungia Aston Villa dakika ya 27, kabla ya Roberto Firmino kuisawazisha Liverpool dakika ya 89.

Liverpool wanafikisha pointi 66 katika mchezo wa 37, ingawa wanabaki nafasi ya tano wakizidiwa pointi tatu na Manchester United ambao pia wana mechi moja mkononi, wakati Aston Villa inafikisha pointi 58 za mechi 37 nafasi ya saba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live