Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Figisu Taifa Stars, Kumbe Shida Ilianzia Airport

Poulsen Kim Poulsen

Sun, 14 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Kim Poulsen wakati akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Madagascar uliochezwa Antananarivo-Madagascar, amesema FIFA na CAF zinasisitiza mchezo wa kiungwana lakini amesikitishwa na namna ambavyo timu imepokelewa Madagascar.

Paulsen anasema shida ilianza tangu ndege ilipotua Madagascar ambapo walichleweshwa kushuka kwenye ndege kwa zaidi ya saa moja na kuanzia hapo bado waliendelea kupata usumbufu.

Kocha anasema kabla ya kutoka Tanzania watu wote walipimwa Corona na kugundulika wapo salama lakini baada ya kupimwa wakiwa Madagascar kuna baadhi ya viongozi wakakutwa na wachezaji wakakutwa na maambuki!

Miongoni mwa wachezaji waliokutwa na Corona kwa mujibu wa vipimo hivyo ni Samatta, Manula na Mwamnyeto. Paulsen anasema wakaenda kuwapima kwenye maabara nyingine lakini majibu yalipotoka yaliknesha wote hawakuwa na Corona.

Kocha anahisi kwamba, wachezaji waliokutwa na Corona ilikuwa ni mpango wa kuidhoofisha timu yake lakini anahoji kuwa maafisa waliowapima hawajui nani ni Samatta au Manula, kwa hiyo kilichofanyika itakuwa ni maofisa wa chama cha soka cha Madagasca na benchi la ufundi ndio walipeleka majina ya wachezaji wanaowahofia ili wabambikiwe maambukizi ya Corona!

Mwisho wa siku Poulsen anasisitiza matokeo ya mchezo yapatikane uwanjani kwa mchezo wa kiungwana lakini pia nje ya uwanja kuwe na uungwana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live